You are currently viewing Wachina kuendesha TAZARA kwa miaka 27, kumwaga trilioni 3.7

Wachina kuendesha TAZARA kwa miaka 27, kumwaga trilioni 3.7


Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Mhandisi Bruno Ching’andu amesema Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) itachukua usimamizi na uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 27 kwa makubaliano yenye thamani ya Dola bilioni 1.4 (Sh trilioni 3.7).

Mha. Ching’andu amesema makubaliano hayo pia yatatoa fursa ya kurekebisha miundombinu ya reli na kuboresha ufanisi wake na kwamba sehemu ya uwekezaji utajumuisha ukarabati wa reli, pamoja na ununuzi wa vichwa vipya na mabehewa.

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni salama na kupanua ufanisi wa reli hiyo yenye uwezo wa usafirishaji wa abiria na mizigo

Mkataba huo wa miaka 30, utalenga kutoa huduma bora na kudumisha operesheni za TAZARA, huku Tanzania na Zambia zikitarajia kuongeza biashara na kuimarisha usafiri wa Mataifa hayo mawili. 

Leave a Reply