You are currently viewing Trump azidi kung’ata, mamia wafutwa kazi usafiri wa nga

Trump azidi kung’ata, mamia wafutwa kazi usafiri wa nga

 Utawala wa Trump umeanza kufuta kazi mamia ya wafanyakazi wa idara ya usafiri wa anga na kusababisha hali ya taharuki kuelekea kwa wikiendi yenye shughuli nyingi za usafiri huo nchini humo.

Hayo yanajiri ikiwa ni wiki chache zimepita baada ya ajali mbaya ya ndege mbili karibu na uwanja wa ndege wa Reagan mjini Washington DC.

Kwa mujibu wa mkuu wa shirikisho la Usalama wa Safari za Ndege, David Spero wafanyakazi waliokuwa wameajiriwa hivi karibuni walikuwa wa kwanza kupata barua pepe Ijumaa wakielezwa kuwa wamefutwa.

Miongoni mwa wafanyakazi waliyoathiriwa ni pamoja na wasimamizi wa mitambo wa FAA, wasimamizi wa kuruka na kupaa kwa ndege kulingana na taarifa ya mmoja wa wafanyakazi ambaye hakutaka kutajwa kwa kuwa hajaruhusiwa kuongea na vyombo vya habari.

Shirikisho la waratibu wa safari za ndege limesema jana Jumatatu kwamba linatathmini athari za usalama wa safari za ndege kufuatia kufutwa kwa wafanyakazi hao.

 Taarifa zimeongeza kuwa wafanyakazi hao wanafutwa wakati tayari kukikuwa na upungufu wa wafanyakazi waliokuwa wakilalamikia kodi za juu na upungufu wa wafanyakazi, pamoja na wasi wasi wa usalama wa safari za ndege.

Leave a Reply