You are currently viewing TRC kununua vichwa vya treni vinavyotumia dizel, umeme

TRC kununua vichwa vya treni vinavyotumia dizel, umeme

Ili kupata suluhisho la kusimama kwa treni itokeapo changamoto ya nishati ya umeme, Shirika la Reli Tanzania limefanya mchakato wa manunuzi ya vichwa vya treni vinavyotumia nishati za umeme na Dizeli (Hybrid locomotives).

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano, Fredy Mwanjala, vichwa hivyo vitatumia umeme na mara itokeapo hitilafu ya njia ya umeme, injini ya dizeli itawashwa na treni kuendelea na safari.

Awali akinukuliwa na gazeti la Citizen, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa pia alithibitisha mpango huo na kuelezea kuwa tayari kampuni moja imebainishwa kuzalisha injini hizo.

“Fedha za kununua injini hizi tayari zimetengwa kwenye bajeti yetu. Mchakato wa ununuzi umeanza, na tunatarajia kununua injini hizo ifikapo mwaka ujao.”

Leave a Reply