You are currently viewing Rungu la CAF latua Simba, kucheza bila mashabiki, faini mil. 100

Rungu la CAF latua Simba, kucheza bila mashabiki, faini mil. 100

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) limeipiga faini ya Sh milioni 100.6 Klabu ya Simba pamoja na kuagiza mechi moja kuchezwa bila mashabiki.

Hatua hiyo imetokana na vurugu zilizojitokeza katika mchezo Simba Sc. dhidi ya CS Sfaxien uliofanyika Disemba 15, 2024.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne na Kaimu Afisa Mtenda Mkuu wa Klabu hiyo, Zubeda Hassa Sakuru imesema uamuzi huo wa CAF umeifungia klabu mechi mbili, hata hivyo adhabu hiyo imepunguzwa kuwa mechi moja kucheza bila mashabiki pamoja na faini ya Dola elfu 40,000.

“Hivyo tunapenda kuufahamisha umma kuwa tunaendelea kufanya taratibu ili kushughulikia uamuzi huo.

“Kwa maamuzi hayo klabu inasitisha mauzo ya tiketi ya mchezo wetu dhidi ya CS Constantine na kwa mashabiki ambao wameshanunua tiketi tunaomba tiketi hizo zitatumika kwenye mchezo ujao wa robo fainali.

 “Klabu ya Simba itaendelea kusimamia taratibu, kanuni na sheria zinazozingatia usalama wa jumla katika michezo,” imesema taarifa hiyo.

Leave a Reply