Rubani wa shirika la ndege la Turkish Airlines amefariki dunia baada ya kuugua ghafla akiwa kwenye ndege kutoka Seattle kwenye pwani ya kaskazini magharibi mwa Marekani kuelekea Istanbul nchini Uturuki.
Captain Ilcehin Pehlivan, 59, alianguka ndani ya ndege angani na rubani wa pili alichukua udhibiti, msemaji wa shirika la ndege alisema kwenye mtandao wa X.
“Huduma ya kwanza kwa nahodha wetu kwenye ndege aliposhindwa, wahudumu wa chumba cha marubani… waliamua kutua kwa dharura, lakini alifariki kabla ya kutua,” Yahya Ustun alieleza.
The Airbus A350 ilitua New York na mipango ikafanywa kuwasafirisha abiria hadi Uturuki , ambapo ndege TK204 ilipaa kutoka Seattle muda mfupi baada ya 19:00 Jumanne jion.
Pehlivan alikuwa amesafiri na shirika la ndege la Turkish Airlines tangu 2007 na alikuwa akipimwa afya mara kwa mara mapema mwezi Machi, ambapo hakupata tatizo lolote la kiafya ambalo lingeweza kuathiri kazi yake, shirika hilo la ndege lilisema.
Chama cha wadhibiti wa usafiri wa anga nchini Uturuki, TATCA, kimesema amehudumia jumuiya ya usafiri wa anga kwa miaka mingi na chama hicho kimetoa toa rambirambi zake kwa familia yake, marafiki na wafanyakazi wenzake.
Chanzo cha kifo cha rubani huyo hakijajulikana. Huku taarifa zikisema Marubani wanapaswa kufanyiwa vipimo vya kimatibabu kila baada ya miezi 12, huku wale wenye umri wa zaidi ya miaka 40 wakilazimika kuhuisha vyeti vyao vya matibabu kila baada ya miezi sita.
Mwaka wa 2015, rubani wa shirika la ndege la American Airlines mwenye umri wa miaka 57 alianguka na kupoteza maisha wakati wa safari ya usiku kutoka Phoenix kwenda Boston. na msaidizi wake wa kwanza alichukua nafasi na kutua kwa dharura huko Syracuse.