You are currently viewing Rais Samia ateta na Mmiliki Machester United

Rais Samia ateta na Mmiliki Machester United

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 11, 2025, amekutana na kufanya mazungumzo na mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya Manchester United yenye maskani yake nchini Uingereza, Sir Jim Ratcliffe, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao Rais Dkt. Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers inayoshughulika na masuala ya Uhifadhi.

Dkt. Samia alisema Taasisi hiyo inafanya vizuri katika kudhibiti muingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).  

Katika kikao hicho, Six Rivers, Sir Jim Ratcliffe amebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhi ya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo.

Leave a Reply