You are currently viewing Rais Samia ataja mwelekeo sekta ya madini nchini
Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ataja mwelekeo sekta ya madini nchini

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema katika kuimarisha manufaa wanayopata Watanzania kupitia sekta ya madini, mwelekeo wa Serikali ni madini hayo kuongezewa thamani hapa nchini, kuwezesha Benki Kuu ya Tanzania kuwa na akiba ya dhahabu, na kuhakikisha kuwa wenye leseni za uchimbaji madini wanazitumia kikamilifu.

Rais Dk. Samia ameyasema hayo leo tarehe 13 Oktoba, 2024 wakati akifunga Maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yaliyofanyika katika viwanja vya Kituo cha Uwekezaji cha Bombambili.

Rais Samia akisalimiana na Buliana Stephano Kidaso mama mzazi wa Mama Janeth Magufuli.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Sharifa  Nyanga pia imesema Rais Dk. Samia amesema ni hatua muhimu kwa wadau kukutana na kubadilishana uzoefu, teknolojia na kupata climu ya fursa zinazopatikana kwenye sekta ya madini katika kuimarisha uwekezaji na kuongeza ushiriki na manufaa kwa Watanzania kupitia sekta hiyo.

Aidha, Rais Dk. Samia amesema Serikali imeanza kutekeleza mpango wa kuhakikisha Tanzania inakuwa na akiba ya kutosha ya dhahabu kupitia wamiliki wa leseni na wafanyabiashara wa madini kutenga asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa nchini na kuiuzia Benki Kuu ya Tanzania.

Daraja la John Magufuli

Awali, Rais Dk. Samia alitembelea kiwanda cha Geita Gold Refinery na Soko la Madini la Geita ambalo ni moja kati ya masoko 44 katika mikoa yote na vituo l03 vya kununulia madini, na kutoa rai kwa wachimbaji wadogo kuendelea kutumia masoko hayo ambayo yanawahakikishia soko la uhakika.

Vilevile, leo Rais Dkt. Samia amekagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la John Magufuli linalounganisha eneo la Kigongo (Misungwi) na Busisi (Sengerema) lenye urefu wa kilomita 3, na kusalimiana na Buliana Stephano Kidaso mama mzazi wa Mama Janeth Magufuli.

Leave a Reply