Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amewateua wakurugenzi, manaibu wakurugenzi, katibu na naibu katibu wa kamati ya itifaki na udhibiti baada ya kushauriana na makamu wenyeviti.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Mwenyekiti huyo, imesema uteuzi huo umezingatia Ibara ya 94(1)(f) ya Katiba ya CUF- Chama Cha Wananchi ya mwaka 1992 Toleo la mwaka 2019,
Amewataja walioteuliwa kushika nafasi zilizoainishwa kwenye Ibara hiyo kuwa ni; Rajab Mbarouk Mohamed- Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti; Juma Wandwi – Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti na Eng. Mohamed Ngulangwa- Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma.
Wengine ni Ali Rashid Ali (Abarani)- Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma; Amina Ali Hamad – Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria; Rashid Mweyo- Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria; Zaynab Amir Mndolwa – Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi na Nawiya Abdallah – Naibu Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi; Hamis Hamad Ibrahim – Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi.
Pia Yusuf Mbungiro ameteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi; Mneke Jafar- Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge, Sera na Utafiti.
Aidha, Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Bunge, Sera na Utafiti atatangazwa baadae.
‘Wakurugenzi wateule wanaanza kazi mara moja na Uteuzi huu utafikishwa kwenye Kikao kijacho cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa ajili ya kuthibitishwa,” amesema.