You are currently viewing Polisi kata wa kata ya Nyigogo – Magu asimikwa uchifu

Polisi kata wa kata ya Nyigogo – Magu asimikwa uchifu

Polisi wa Kata, Makoye Kitula katika Kata ya Nyigogo iliyopo katika wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambaye pia Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi amesimikwa uchifu na kupewa jina la Chifu Kalikali.

Zoezi hilo limefanyika jana tarehe 2 Januari 2025 katika Kijiji Cha ilugu wakati wa sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya 2025, sherehe hiyo iliwashirikisha wazee na waganga wa jadi wa eneo hilo.

Kitula amewashukuru wananchi wa Nyigogo kwa kutambua mchango wake katika maswala ya ulinzi na usalama na kuahidi atafanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kauli mbiu ya jeshi la Polisi isemayo Nidhamu, haki, weledi na uadilifu.

Kwa upande Mathias Magashi Mwenyekiti wa waganga wa jadi Kata ya Nyigogo amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu pia kuwafichua waganga wanaopiga ramli chonganishi.

Leave a Reply