You are currently viewing Mbunge Wanu Ameir akabidhi kisima cha maji Makunduchi

Mbunge Wanu Ameir akabidhi kisima cha maji Makunduchi

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Wanu Hafidh Ameir jana tarehe 22 Machi, 2025 amekabidhi kisima cha maji katika Kijiji cha Miwaleni Makunduchi kitakachosaidia kutatua changamoto ya maji kijijini hapo.

Itakumbukwa kuwa, jana tarehe 22 Machi, 2025 ilikuwa ni siku ya kuadhimisha Wiki ya Maji Duniani (World Water Day) iliyokuwa na *Kauli Mbiu: Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji*

Kwa upande wake, Wanu Hafidh Ameir amesema kuwa, amekabidhi kisima cha maji ili kiwe kama sadaka kwa wakazi wote wa Kijiji cha Miwaleni Makunduchi ili kuwatoa watu katika shida na dhiki ya kuhangaika na maji.

Aidha, Wanu amesisitiza wananchi kuwa na utunzaji mzuri wa vyanzo vya maji sambamba na matumizi sahihi ya miundombinu ya maji ili miundombinu iendelee kunufaisha wananchi kwa muda mwingi.

Screenshot

Vilevile, Wanu amesema kuwa, ataendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kijijini Miwaleni Makunduchi na maeneo mengine na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuwa na afya bora 

Aidha, wananchi wa Makunduchi wamemshukuru Mwenyekiti wa MIF, Wanu kwa kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwatumikia kwani miradi mingi ya maendeleo imewafikia katika kipindi cha uongozi wake, ikiwemo miradi ya sekta ya maji

Leave a Reply