You are currently viewing Lissu alegeza masharti Chadema kushiriki uchaguzi mkuu

Lissu alegeza masharti Chadema kushiriki uchaguzi mkuu

Mwandishi Wetu, Ruvuma

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amelegeza masharti kuhusu chama hicho, kushiriki uchaguzi akitaka mambo sita yafanyikie ili waingie katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Lissua ametaja mambo hayo ni kubadilishwa kwa mfumo wa uchaguzi ili kusiwe na mgombea anayepita bila kupingwa, watoto wadogo wasiandikishwe kwenye daftari la kudumu la mpigakura, kukomeshwa engua engua ya wagombea wa upinzani

Kwa mujibu wa Lissu, mengine ni wagombea wa upinzani wasifanyiwe vurugu kwenye kampeni, mawakala hasa wa vyama vyote wafanye shughuli zao bila usumbufu na uchaguzi usiwe sehemu ya kutoa kafara ili kupata viongozi.

Lissu alieleza hayo jana Jumanne wakati akizungumza na wananchi wa Namtumbo mkoani Ruvuma, akitokea wilaya za Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara katika mwendelezo wa ziara ya chama hicho, kunadi ‘No Reforms No Election.

Masharti haya aliyotoa Mwenyekiti Lissu hayajajumuisha mambo makubwa ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele hapo awali hususan mabadiliko ya kisheria kuruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani, wakurugenzi wa halmashauri kutosimamia uchaguzi, na Rais kutokua na sehemu ya mchakato wa uteuzi wa mwenyekiti wa tume na makamishna wa uchaguzi. 

Mambo sita aliyotaja Lissu hayahitaji mabadilikop ya kisheria na mengi tayari yamezingatiwa katika sheria zilizopo na mabadiliko ya sheria za uchaguzi yaliyofanyika kupitia kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2023 na Rais Dk Samia Suluhu Hassan. Kwa mfano, kila anayeandikishwa kupiga kura lazima awe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea, huku ikiwa ni marufuku mgombea kupita bila kupingwa (kura ya ndio na hapana). 

Masharti haya mepesi na mapya ya Lissu yanaweza kuwa ni safari mpya ya kukiandaa Chama chao kubadili msimamo wa no refoms no election, ili Kwenda katika utiliaji saini wa kanuni za Uchaguzi zinazotarajiwa kufanyika Aprili 12 kama maandalizi ya kushiriki uchaguzu mkuu.

Leave a Reply