You are currently viewing Kongo yaitaka Rwanda kulipa fidia ya vita

Kongo yaitaka Rwanda kulipa fidia ya vita

Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu, imeanza kusikiliza shauri lililowasilishwa mahakamni hapo na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo dhidi ya Rwanda, kuhusu mgogoro wa kivita wa muda mrefu mashariki mwa Congo.

Jopo la wanasheria wa Rwanda wameiambia mahakama kuwa kesi hiyo inahusisha masuala ya mizozo ya kijeshi na siasa za kikanda.
Rwanda ikifafanua zaidi kwamba mizozo hiyo ni nje ya wigo wa mamlaka ya mahakama hiyo.

Upande wa waleta maombi Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, unasema madai ya Rwanda yanapotosha sheria na itifaki ya Mahakama, na inapaswa kuwajibishwa kwa makosa iliyoyafanya.

Samwel Mbemba Kabuya ambaye ni wakili upande wa waleta maombi alisema, “Kesi hii ni muhimu kwetu Congo kutokana na machafuko yaliyotokea, vifo vya mamilioni ya watu na machafuko yanayoendelea mpaka sasa. Tunataka Mahakama ichukue hatua kwa Rwanda, wawajibike kwa makossa waliyoyafanya na haya mambo yasitokee tena.”

Kesi hii namba saba ya mwaka 2023, inatarajiwa kusikilizwa tena Kesho ambapo mahakama itatoa maamuzi dhidi ya madai ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Leave a Reply