You are currently viewing Aweso atua Korea kusaka teknolojia za upotevu wa maji nchini

Aweso atua Korea kusaka teknolojia za upotevu wa maji nchini

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso amewasili Seoul nchini Korea Kusini kwa mualiko maalumu wa Benki ya Exim ya Korea na mfuko wa mashirikiano ya kiuchumi wa Korea (EDCF) ambapo anatarajia kukutana na Makamu wa Rais wa Benki hiyo tarehe 06 Desemba 2024 kujenga mashirikiano zaidi baada ya uwekezaji wa serikali ya Korea kusini katika miradi ya Maji Taka kwa Majiji ya Dar Es Salaam, Dodoma na Manispaa ya Iringa.

Waziri Aweso amepokelewa na mwenyeji wake Togolani Edriss Mavura, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Korea Kusini.

Aidha, Waziri Aweso akiwa Seoul Korea, ametembelea moja ya makampuni makubwa ya Teknolojia katika Sekta ya Maji ya nchini Korea ya Green Tech. Inc ambayo imefunga mfumo wa mita janja (Smart Water Managemant System) katika Manispaa 43 nchini humo pamoja na nchi nyingine,ili kujionea Teknolojia hiyo pamoja na kuona namna mfumo huo unavyofanya  kazi.

Waziri Aweso amesema Mamlaka ya Maji ya Iringa IRUWASA imepanga kufunga “mfumo janja wa kusimamia Menejiment ya usambazaji maji” Mjini Iringa (Smart Water Management System). 

Mradi huu utawezesha kupunguza upotevu wa Maji na kusimamia ubora na msukumo wa maji katika mfumo wote wa usambazaji kupitia mfumo maalumu wa mawasiliano.

Leave a Reply