You are currently viewing Wadau TPA waridhishwa na huduma bandari nchini

Wadau TPA waridhishwa na huduma bandari nchini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WADAU mbalimbali na watumiaji wa huduma za bandari wameridhishwa na ubora wa huduma  sambamba na  utendaji kazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) wakisema mamlaka imefanikiwa kukidhi matarajio ya wateja wake  pamoja  kuyafikia malengo iliyojiwekea.

Wakizungumza katika kilele cha wiki ya huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam jana, mmoja wa wadau hao Hassini Norana ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia uwekezaji katika Bandari ya Dar e Salaam.

“Huduma za bandari zimeimarika sana sambamba na kuwepo kwa ufanisi mkubwa. Ninaipongeza TPA kwa kufanyanya maboresho makubwa,” alisema Norana na kuitaka TPA kuendelea kuzitangaza bandari zake.

Naye Mdau wa kutoka Bandari Kavu, Deogratius Chacha alipongeza ufanisi na utendaji uliopo kwenye Bandari ya Dar es Sslaam na kuipongeza menejimenti ya mamlaka hiyo kwa maboresho makubwa.

“Uwekezaji mkubwa uliofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na zile zilizopo kwenye maziwa ni Ushahidi tosha kuwa TPA imejipanga vizuri kuleta mageuzi makubwa kwenye bandari zake,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt George Fasha aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu kwenye hafla hiyo ya kilele, Plasduce Mbossa amewashukuru wadau na watumiaji wote wa bandari kwa kuendelea kuiamini na kutumia bandari zilizopo hapa nchini.

“Nikiri kuwa TPA tunauthamini sana mchango wenu kwani ni moja ya chachu inayofanikisha maendeleo ya mamlaka bna taifa kwa ujumla wake,” alisema na kuongeza kuwa TPA imefanya maboresho makubwa nay a kisasa katika bandari zote.

Dkt Fasha amesema TPA kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 imeweza kuhudumia meli 4,487 na zilikuwa na jumla ya shehena milioni 27.6 ambapo katika shehena hiyo makasha yalikuwa milioni 1,1 na kuhudumiwa katika terminal zote mbili sambamba na Bandari za Tanga na Mtwara.

“Pamoja hayo Mamlaka bado imeelekeza juhudi zake katika kuboresha miundombinu ya bandari zote ili kukidhi mahitaji ya soko linalobadilika na kukua kwa kasi huku likiwa na ushindani mkubwa toka bandari shindani,” alisema.

Dk. Fasha alisema bado maboresho mbalimbali yanaendelea ikiwemo kujenga gati la mita 450 kwenye Bandari ya Tanga kwa jumla ya gharama ya bilioni 429.1 na kuondoa tatizo la ‘double handling’ na pia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam.

Dk. Fasha pia alibainisha kwa wateja kuwa TPA ina mipango na mikakati kabambe ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kuhifadhi mafuta ili kupunguza muda wa kuhudumia meli nangani kutoka siku 8 hadi 10 mpaka kufika siku tatu kwa meli zenye ujazo wa  150,000 DWT na kupunguza gharama za ucheleweshaji wa meli.

“Kuanza ujenzi  Gati namba 12 hadi 15 katika Bandari ya Dar es Salaam ilikukabiliana na uhaba na Magatii li Kwenda sambamba  na ongezeko la meli na shehena. Gati hizo zilikuwa na uwezo wa kuhudumia makasha 1,350,000 kwa mwaka sawa na kujenga tani milioni 31.05,” aliongeza.

Leave a Reply