You are currently viewing Watatu wakamatwa wakisafirisha dhahabu ya Mil 750 kwa magendo

Watatu wakamatwa wakisafirisha dhahabu ya Mil 750 kwa magendo

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu watatu waliokamatwa wakiwa na gramu 3263.72 za dhahabu yenye thamani ya shilingi milioni 749.5

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatano na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi ( ACP) Adam Maro, watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha kwa njia za magendo dhahabu hiyo kinyume cha sheria.

Amesema watuhumiwa hao walisafirisha kwa kutumia gari aina ya Toyota Premio yenye namba za usajili T.739 EEH mali ya Emanuel Kidenya Mkazi wa Kahama, Shinyanga.

Amewayaka waliokamatwa ni Yohana ldama (34), Mkazi ya Nyamhongolo wilaya ya Ilemela Mwanza, Moshi Manzili (26), Mkazi wa Bariadi Simiyu na Hamidu Salum (25), Mkazi wa Nyasubi wilaya ya Kahama Shinyanga.

“Watuhumiwa hao wamekamatwa Machi 24, 2025 majira ya saa 5 usiku katika Mtaa wa Kapera Wilayani Bukombe baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri na kuweka mtego uliofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hawa. 

“Baada ya upekuzi wa gari kufanyika, walikutwa wakiwa na kiasi hicho cha dhahabu kilichokuwa kimefichwa ndani ya gari hiyo.

“Uchunguzi wa tukio hili kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine unaendelea kufanyika sambamba na kubaini na kuwakamata watakaobainika kujihusisha na uhalifu huo na kuwafikisha Mahakamani mara moja,” amesema.

Leave a Reply