You are currently viewing RITA kuwanoa wajumbe  bodi, taasisi za wadhamini Dar 

RITA kuwanoa wajumbe  bodi, taasisi za wadhamini Dar 

Na Mwandishi Wetu, Dar ves Salaam

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeandaa mafunzo maalum kwa wajumbe   wote wa Bodi za Wadhamini wa Taasisi zilizosajiliwa RITA zilizopo Dar es Salaam  yakayofanyika  kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Kumbumbuku ya Mwalimu Nyerere  Jijini kesho Jumatano.

Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wa  kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa  RITA, Bw Frank Kanyusi aliwataka wajumbe wote kukamilisha kujisajili kwa ajili ya kushiriki  kwenye mafunzo hayo Maalum  yaliyondaliwa na taasisi yake ambapo  Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

“Wadhamini watakaoshiriki mafunzo hayo maalum watatakiwa kujisajili kupitia kiunganishi kifuatacho https:tsms.gov.go.tz/login na watakaoshiriki watapata fursa ya kupata miongozo ya jinsi ya kupata huduma mbalimbali ikiwa pamoja na kufanya marejesho kwa mfumo wa kidijitali wa eRITA,” alisema Bw Kanyusi.

Bodi za wdhamini ni pamoja na  Vyama vya Siasa, Taasisi na Madhehebu ya kidini, Vyama/Vilabu vya michezo, Taasisi binafsi za kijamii zilizo na wanachama na zinazomiliki mali na  Vyama vya Kiuchumi.

Bw Kanyusi amesema  kwa mujibu wa Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini Sura ya 318 Toleo la 2002 ni mtu yeyote au wanachama wa Taasisi aliyepewa mamlaka au nafasi ya uaminifu ya kusimamia mali kwa faida ya wanachama/walengwa kisheria kwa malengo/madhumuni yaliyoainishwa.

“RITA ina matumaini kwamba  baada ya mafunzo hayo, tunatarajia masuala ya  ubadhirifu, matumizi mabaya ya Madaraka na migogoro itapungua au kuisha kabisa hivyo Taasisi hizo kuweza kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.,” alisitiza.

Aliseman RITA imesajili taasisi zaidi ya 4,300  nchini kote  ambapo zaidi ya asilimia 65 ya taasisi hizo zipo Dar es salaam  na hivyo kuwataka wadhamini hao wajitokeza kwa wingi kuhudhuria mafunzo hayo muhimu kwa ustawi wa taasisi zao.

“Chimbuko la Mkutano huo ni matokea ya ziara ambazo Wakala umefanya kuzitembelea taasisi hizo na kubaini sehemu kubwa ya wadhamini hawana ufahamu wa kutosha wa majukumu na wajibu wao katika kusimamia mali za taasisi zao hivyo kushindwa kuzisimamia ipasavyo.,” amesema Bw Kanyusi na kuongeza kuwa wapo wadhamini ambao kwa kujua au kutokujua wamekuwa wakikiuka misingi na Katiba za taasisi zao na kusababisha migogoro na ubadhirifu wa mali.

Leave a Reply