Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameeleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa kwenye mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Arusha.
Uwanja huo ambao umefikia 28% ya ujenzi, ni saw ana asilimia tatu zaidi ya kile kilichokusudiwa kwa wakati huu wa miezi 7 tangu kuanza kwa ujenzi.
Kabudi amesema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo unaojengwa katika kata ya Olmoti jijini Arusha ambapo Uwanja huo unatarajiwa kutumika katika mashindano ya AFCON 2027.