Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa Wizara na nchi kwa pamoja imeamua kufanya muziki wa Singeli kuwa alama ya Mtanzania kwa kupeleka kwenye nchi mbalimbali ili kuukuza muziki huo.
Waziri Kabudi ameyasema hayo leo Februari 17, 2025 jijini Dar es Salaam alipotembelea Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu mustakabali wa sanaa nchini ambapo ameeleza kuwa muziki huo wenye vionjo vya kitamaduni utakuwa moja ya alama na utambulisho wa Tanzania kimataifa.