You are currently viewing Rais Tshisekedi akataa mazungumzo na M23

Rais Tshisekedi akataa mazungumzo na M23

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi ameondowa uwezekano wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la M23, akisema kwamba hatua hiyo italipa uhalali kundi hilo.

Kauli hiyo inajiri baada ya mkutano uliotarajiwa  kufanyika tarehe 15 Disemba nchini Angola kati ya Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame kufutwa wakati pande hizo mbili hazikuweza kukubaliana kuhusu masharti ya mazungumzo hayo.

Tshisekedi aliwaambia wanadiplomasia mjini Kinshasa kwamba mazungumzo hayo yameshindwa kwa sababu ya ujumbe wa Rwanda kutowa sharti jipa la kutaka  yafanyike mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi la M23.

Siku ya Alhamisi, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Rais wa Angola Joao Lourenco walitoa wito wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo katika ngazi ya juu kati ya DRC na Rwanda. Lakini Tshisekedi alisema nchi yake haitakubali kile alichokitaja kama “shinikizo kutoka nje” kuweka masharti ambayo yanakiuka kanuni na mamlaka ya Kongo.

Leave a Reply