Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuhakikisha wanatumia nishati safi ya kupikia kama njia mahususi ya kutunza na kulinda mazingira pia kuokoa uharibifu wa misitu.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo tarehe 31 Disemba 2024 kKatika tamasha maalumu la azimio la Kizimkazi lililofanyika mkoani Lindi wilaya ya Ruangwa.
![](https://www.mchukuzitv.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/f55da117-4538-448d-8118-f465657703b1-1024x576.jpeg)
Amesema uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kimataifa inayofanyika kwa lengo la kuimarisha afya za wananchi na kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati endelevu.
![](https://www.mchukuzitv.co.tz/wp-content/uploads/2024/12/2ca51570-b381-4d85-b01a-2d1e0b4d31e0-1024x682.jpeg)
Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Baada ya jumuiya za kimataifa kuanzisha kampeni hii Rais Samia Suluhu Hassan alikuwa wa kwanza kuibeba na kuileta nchini Tanzania kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa vitendo jambo ambalo limeongeza msukumo na kukuza matumizi ya nishati safi hasa katika maeneo ya vijijini”