Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa ya ufugaji wa sungura kutokana na kuwapo kwa soko la wanyama hao nchini na duniani.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhan Kyande wakati wa mafunzo ya ufugaji sungura kwa watumishi wa Magu yaliyoendeshwa na kampuni ya uwekezaji ya Saore Company Limited.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri Desemba 06, 2024 Kyande amesema kwa sasa sungura wana soko kubwa nchini na duniani kwa ujumla na ufugaji wake hauna gharama kubwa.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka kampuni ya Saore amesmea Jacline Charles amesema mnyama huyo ana fursa nyingi endapo mfugaji atazingatia maelekezo wakati wa kumfuga mnyama huyo kwani sungura wanazaliana na kwa wingi.
Amesema mbali na kuvuna nyama ya sungura pia kuna fursa nyingine kama vile mkojo wa sungura na kinyesi kutumika kama mbolea .