You are currently viewing TPA mwajiri bora sekta ya umma 2024

TPA mwajiri bora sekta ya umma 2024

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Usimamizi waBandari Tanzania (TPA) kwa mara ya tatu mfululizo imetangazwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kuwa ni mwajiri bora wa sekta ya umma na kupewa Tuzo ya Mwanachama wa Kudumu kwa Taasisi za Umma.

Akikabidhi uongozi wa TPA tuzo za umahiri mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salamaa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, amewapongeza wafanyakazi na viongozi wa TPA kwa ushindi wa tuzo hizo.

Pia ameitaka mamlaka kuendeleza juhudi ambazoo zimeifanya ishinde tuzo mara tatu mfululizo.  

Dk Biteko amekumbusha kwamba TPA ni taasisi ya kitaifa ya kiuchumi na kimkakati na kueleza furaha yake kwa utendaji wa TPA ambao umetambuliwa  na ATE pasipo upendeleo wowote.  

Alisema TPA siyo tu inafanya vizuri kiuchumi bali imeonyesha kwamba ni mwajiri wa kupigiwa mfano nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala, Mbarikiwa Masinga (kulia), na Meneja Rasimali Watu, Mussa Mzenga (kushoto) mara baada ya kuoabidhiwa tuzo ya mwajli bora wa mwaka sekta ya umma, tuzo ya mwajili bora mzawa, tuzo ya mshindi wa watu wa jumla sekta zote,tuzo ya wanaofanya vizuri zaidi na tuzo ya mwanachama wa ATE wa muda mrefu

Dk. Biteko alimwakilisha Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango katika hafla hiyo na kuwafikishia wafanyakazi na uongozi wa TPA salamu za Makamu wa Rais za kuwatakia mafunikio katika siku zijazo.

Naibu Waziri Mkuu aliwaelezwa kwamba TPA haikushinda tu Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka katika sekta ya umma, bali pia imetwaa tuzo nyingine nne ikiwemo Tuzo ya Mwajiri  Bora Mzawa (Local Employer Award), mamlaka ikiwa mshindi wa kwanza; TPA pia ilitangazwa kuwa mshindi wa pili wa jumla kwa sekta zote na kupewa Tuzo ya 2nd Runners-Up.

Aidha, TPA ilitambuliwa  kama moja ya taasisi zinazofanya vizuri sana na kupewa Tuzo ya Club of Best Performers na kupongezwa kwa uanachama wa muda mrefu  wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kupewa Tuzo ya Mwanachama wa Kudumu kwa Taasisi za Umma.

Dk. Biteko alifahamishwa kuwa tuzo hizi hutolewa kila mwaka na ATE kwa waajiri kutoka sekta za umma na binafsi ambao wameonyesha utendaji bora na ubunifu katika mwaka husika. 

Ilielezwa kuwa ushindi wa TPA ni uthibitisho wa dhamira yake ya kuboresha ustawi wa wafanyakazi, kuboresha mazingira ya kazi na kuendelea kuchangia maendeleo ya sekta ya bandari nchini.

Mwaka huu TPA ilitowa kwa serikali gawio la Sh. bilioni 153.9 na kuwa taasisi iliyotoa gawio la juu kabisa.  

Kampuni 145 zilikabidhi kwa Rais Samia Suluhu Hassan jumla ya shilingi bilioni 636 ikiwa ni gawio kwa serikali. Taasisi za kibiashara zilitoa 278bn/- na mamlaka za udhibiti zilitoa 358bn/-.

Leave a Reply