You are currently viewing Haya hapa matokeo ya mtihani wa darasa la saba (PSLE) 2024

Haya hapa matokeo ya mtihani wa darasa la saba (PSLE) 2024

BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) leo tarehe 29 Oktoba, 2024 limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba ambayo yanaonesha kuwa jumla ya watahiniwa 974,229 sawa na 80.87%, watahiniwa wenye matokeo wamefaulu na kumaliza Elimu ya Msingi 2024.

Katibu Mtendaji wa NECTA, Said Mohamed

Akitangaza matokeo hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Said Mohamed amesema ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.29%.

Amesema kati ya watahiniwa hao wavulana ni 449,057 sawa na 81.85% na wasichana ni 525,172 sawa na 80.05%, hivyo ufaulu wa wasichana umeshuka kwa 0.53% na ufaulu wa wavulana umeongezeka kwa 1.26%.

Bofya hapa kutazama matokeo ya mtihanin wa darasa la saba. https://matokeo.necta.go.tz/results/2024/pslexj6/psle.htm

Leave a Reply