You are currently viewing  RC Chalamila akagua mradi BRT Bagamoyo, atoa maagizo kwa wakandarasi

 RC Chalamila akagua mradi BRT Bagamoyo, atoa maagizo kwa wakandarasi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo ya mwendokasi inayounganisha maeneo ya Tegeta, Mwenge, Ubungo na Mbezi na kuwataka wakandarasi kutekeleza kwa ufanisi mradi huo unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi nane.

Mradi huo hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 61 ya ukamilifu na inaelezewa kuwa itakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Bunju na maeneo jirani kwa kuboresha huduma za usafiri.

Chalamila ametoa maagizo hayo wakati akiendelea na ziara yake ya usiku kwa usiku jana tarehe 23 Oktoba, 2024, ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya ukaguzi  wa miundombinu na utoaji wa huduma nyakati za usiku katika Wilaya ya Kinondoni.

Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa ametembelea Shule ya Sekodari Mabwe Tumaini na kuzungumza na wanafunzi, akiwahimiza kusoma kwa bidii kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameboresha mazingira ya kujifunzia.

Aidha, amewataka kuepuka vitendo viovu shuleni. RC Chalamila pia ameahidi kuwazawadia wanafunzi mchele, ng’ombe, na soda vilevile shilingi laki 3 kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya mpira wa kikapu.

Akiwa ziarani humu RC Chalamila amepita kukagua mwenendo wa utendaji kazi katika kituo cha polisi cha mabwepande.

Ametoa maagizo ya kutomchekea mtu yeyote anayedhamiria kuharibu amani ya nchi yetu na kushughurika na wavunjifu wa amani kama wezi,vibaka, sambamba na sheria za nchi na kushughulikia biashara haramu zinazoingia nchini kwa magendo kama madawa ya kulevya.

Mwisho wa ziara hiyo ya usiku wa kuamkia tarehe 24 Oktoba ametembelea pia hospitali ya Wilaya ya Mabwepande iliyojengwa zaidi ya milioni 400 ghorofa tofauti tofauti zilizomo kituoni humo.

“Sekta ya afya ni sekta muhimu na haihitaji siasa, watoa huduma za afya wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.

Leave a Reply